Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha ustahimilivu wa taifa dhidi ya majanga, kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati na miradi mbalimbali.
Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuendelea kujenga ustahimilivu wa jamii dhidi ya maafa, na hivyo kuokoa maisha, mali, na rasilimali za taifa letu.
Amesema hayo leo, Jumatatu, Oktoba 13, 2025, wakati akitoa tamko katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa City Park Garden, jijini Mbeya.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates