Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso, amewataka wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa ni watu wenye sifa na uwezo wa kuleta maendeleo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, jimbo la Kigoma Kaskazini, Paresso amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kuwachagua viongozi wa CCM.

Amesema chama hicho kimejipanga kushinda kwa kuwa kimeleta wagombea bora wanaoendana na mahitaji ya Watanzania.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *