Kundi lenye mfungamano na Islamic State, ADF, inashtumiwa kutekeleza shambulio lililogharimlu maisha ya wayu wasiopunguwa 19 katika kijiji cha Mukondo, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia. Mauaji hayo yanayobainisha kutokuwa na uwezo wa mamlaka kulinda wakazi wa mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Takriban watu kumi na tisa waliuawa katika shambulio la Allied kndi la waasi wa Uganda la ADF usiku wa Jumapili, Oktoba 12 kuamkia Jumatatu, Oktoba 13, katika kijiji cha Mukondo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo kundi hili lenye silaha limekuwa likifanya mfululizo wa mauaji ya raia.

Waasi walitekeleza shambulio katika kijiji hiki, kilicho katika eneo la Lubero, na “kuwachinja watu kumi na tisa,” Kanali Alain Kiwewa, mkuu wa kijeshi wa eneo hilo, ameliambia shirika la habari la  Agence France-Presse (AFP). “Nyumba na maduka kadhaa yalichomwa moto” na “watu wengi waliyahama makazi yao,” ameongeza.

Ni kaskazini mwa eneo linalodhibitiwa na kundi la M23 ambapo ADF, kundi lililoundwa na waasi wa zamani wa Uganda na ambalo lilitangaza utiifu kwa kundi la Islamic State, linafanya mauaji ya mara kwa mara, katika maeneo ya kaskazini mwa mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Mnamo mwezi Septemba, wapiganaji wa Allied Democratic Forces waliua zaidi ya watu 89 katika mashambulio kama hayo. Kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP, raia 180 wameuawa tangu mwezi Julai.

Mamlaka ilikuwa imeonywa juu ya hatari ya kushambuliwa.

Huko Mukondo, raia kumi na sita na askari mmoja wa Kongo walitambuliwa kati ya wahasiriwa; Watu kadhaa pia walitekwa nyara na washambuliaji, Kambale Maboko, kiongozi wa shirika la kiraia la eneo hilo, ameliambia shirika la habari la AFP. “Kulikuwa na maonyo lakini hayakuzingatiwa, angalia sasa matokeo,” amelalamika, akibainisha kuwa mamlaka ilionywa juu ya hatari hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *