Wakati kundi jipya la wahamiaji waliohamishwa kutoka Marekani wakiwasili mjini Accra siku ya Jumatatu, Oktoba 13, ofisi ya mawakili imewasilisha malalamiko katika mahakama ya juu zaidi ya Ghana ikitaka kusimamishwa kwa makubaliano hayo. Ofisi ya mawakili inabaini kwamba mkataba huo sio tu kwamba unakinzana na mikataba ya kimataifa ambayo Ghana imetia saini, lakini kuuidhinisha kwake na Bunge kunasababisha serikali kufanya kazi nje ya mfumo wowote wa kikatiba.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Accra, Victor Cariou

Kundi jipya la wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani liliwasili Ghana asubuhi ya Jumatatu, Oktoba 13. Ndege aina ya Boeing 767-200 waliyokuwa wakisafiria kutoka Baltimore ilitua muda mfupi kabla ya saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ghana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka katika mji mkuu wa Ghana.

Je, ni wangapi, na ni wa mataifa gani? Wakati Bw. Oliver Barker Vormawor, wakili wa Ghana aliyetoa taarifa kwa RFI, alisema kuwa kwa sasa hana maelezo kuhusu suala hili, mamlaka ya Ghana haijajibu ombi letu. Katika hatua hii, wamekubali tu kupokea raia 14 wa Afrika Magharibi waliofukuzwa kutoka Marekani tangu Septemba 10, tarehe ambayo mkataba wa uhamiaji kati ya Accra na Washington ulirasimishwa.

Kundi hili jipya la wahamiaji waliofukuzwa nchini Marekani na kupelekwa nchini Ghana ni la tatu, kulingana na Bw. Oliver Barker Vormawor, ambaye anadai kuwa kundi jingine, linalojumuisha wahamiaji 14, pia liliwasili nchini humo mwezi wa Septemba.

Wakati makubaliano haya kati ya serikali ya Marekani na Ghana yakikabiliwa na ukosoaji mkali, wakili huyo ameamua kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Juu ili litangazwe kuwa ni batili. Pia siku ya Jumatatu, Oktoba 13, aliwasilisha malalamiko katika mahakama ya juu zaidi ya Ghana, akihoji kwamba makubaliano hayo yamezua matatizo mawili hasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *