#HABARI: Mgombea ubunge Jimbo la Kalambo mkoani Rukwa ndugu Edfonce Kanoni, amesema endapo akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anaishauri Serikali kupunguza bei za pembejeo za kilimo ili kuwawezesha wakulima kulima kwa tija.
Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi kupitia mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Viijiji vya Lolesha, Mbuluma, Singiwe na Namlangwa na kusema endapo akichaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha anaishauri Serikali kuongeza fedha za ununuzi wa mazao ikiwa ni pamoja na kupunguza bei ya pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea na mbegu.