Hamas iliwaachilia mateka wa mwisho wa Israel kutoka Gaza Jumatatu chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano, na Israeli iliwarudisha nyumbani mabasi ya wafungwa wa Kipalestina, huku Rais wa Marekani Donald Trump akitangaza kumalizika kwa vita vya miaka miwili Mashariki ya Kati.
Saa kadhaa baadaye, Trump aliwaita viongozi wa Kiislamu na Ulaya nchini Misri kujadili mustakabali wa Ukanda wa Gaza na uwezekano wa kupatikana kwa amani ya eneo hilo, hata kama Hamas na Israel, zote hazikuwepo kwenye mkutano huo, bado hazijakubaliana juu ya hatua zinazofuata.
Jeshi la Israel limesema limepokea mateka wote 20 waliothibitishwa kuwa hai, baada ya kuhamishwa kutoka Gaza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Tangazo hilo lilisababisha kushangiliwa, kukumbatiana na kulia miongoni mwa maelfu ya watu waliokuwa wakisubiri kwenye uwanja wa “Hosta Square” huko Tel Aviv.
Huko Gaza, maelfu ya jamaa, wengi wakilia kwa furaha, walikusanyika katika hospitali ambapo mabasi yaliwarudisha nyumbani baadhi ya wafungwa 2,000 wa Kipalestina na waliokuwa wanazuiliwa na Israel kama sehemu ya makubaliano hayo.
“Anga ni shwari, bunduki ziko kimya, ving’ora vimetulia na jua linachomoza kwenye ardhi ambayo hatimaye imepata amani,” Trump aliambia Knesset, bunge la Israeli, akisema “jinamizi” kwa Waisraeli na Wapalestina limekwisha.
#Chanzobbcswahili
#StarTvUpdate