IRAN vs TANZANIA: “Ni fursa kwa wachezaji wetu kwenda kujionesha”
Mchambuzi wa soka @akingamkono anasema mechi ya leo ya kirafiki kati ya Iran dhidi Tanzania, jambo zuri kwa wachezaji wa Stars kujionesha kimataifa kwasababu kwa eneo wanalokwenda kuchezea, ni rahisi mawakala kwenda kuangalia mechi.
Mbali na wachezaji, lakini pia kwa taifa, viwango vya soka vitapanda kwasababu tunayekwenda kucheza nae ni mkubwa katika soka.
Kwa upande wake mchambuzi @adrianojames_ anasema mechi kama hizi zinatoa fursa kwa Kocha Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ kutengeneza muunganiko kwa wachezaji ambao huwa hawapati nafasi ya kutosha.
Taifa Stars leo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao Iran na mechi hiyo itakuwa LIVE #AzamSports1HD saa 12:00 jioni.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Viwanjani