Kulingana na tovuti ya idara ya mahakama ya Iran, Mizan, mmoja wa watu hao ambao hawakutambulishwa, amefungwa miaka sita jela kwa kosa la kufanya ujasusi, miaka mitano kwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu dhidi ya usalama wa taifa na miaka ishirini kwa kushirikiana kiintelijensia na kile walichokiita utawala wa Kizayuni.

Mtu  wa pili amehukumiwa miaka kumi jela, miaka mitano na mingine 17 kwa makosa sawa na hayo ya mshukiwa wa kwanza.

Tovuti hiyo imesema watu hao wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika kipindi cha siku 20. tangazo hili linakuja mwezi mmoja baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araghchi kusema kuwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa wa Ufaransa na mwanamke wa Iran anayeshikiliwa Ufaransa yanaelekea kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *