Tovuti ya Drop Site News, chombo cha habari cha uchunguzi kilichoko Washington kimefichua kuwa, jeshi la Israel lilichoma kinyama nyumba na vyakula kabla ya kukimbia Ukanda wa Ghaza na baadaye kusambaza picha za unyama huo kwa majivuno na kiburi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Shirika la habari la Tasnim limenukuu taarifa ya tovuti hiyo ya Marekani ikisema kuwa, wakati jeshi la Israel lilipolazimishwa kuondoka Ukanda wa Ghaza lilianza kuteketeza kila kitu hasa chakula ili Wapalestina wanaorejea kwenye maeneo yao waendelee kufa kwa njaa. 

Kwa upande wake televisheni ya Al-Mayadeen imenukuu ripoti ya tovuti hiyo ya Drop Site News ya Marekani ikisema kuwa, jeshi la Israel lilianzisha kwa makusudi wimbi la moto uliochoma na kuteketeza miundombinu ya raia kwenye mji wa Ghaza mara baada ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jinai hiyo ni sehemu ya sera ambayo jeshi la Israel limekuwa likizitekelezwa Ghaza katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, yaani kuchoma na kuharibu makazi ya raia na miundombinu ya kiraia.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, usiku wa Oktoba 9 na alfajiri ya Oktoba 10, mara baada ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kabla ya kuridhiwa na baraza la mawaziri la Israel, Mji wa Gaza ulishuhudia wimbi kubwa zaidi la moto ambalo halijawahi kushuhudiwa katika kipindi chote cha miaka miwili ya vita na mauaji ya umati ya Israel huko Ghaza.

Jeshi la Israel pia limesambaza makumi ya picha na video za majengo yaliyokuwa yakiteketea kwa moto katika Jiji la Ghaza wakati wanajeshi hao makatili wasio na chembe ya utu walipokuwa wanaondoka mjini humo huku wakiona fakhari kusambaza uharibifu na jinai hizo kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *