Kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la Anadolu, CAPSAT ilichukua hatua hiyo baada ya Bunge kupitisha azimio la kumuondoa madarakani Rais Rajoelina.

Kikosi cha CAPSAT, kikiongozwa na Kanali Michael Randrianirina, kiliingia katika Ikulu ya Ambohitsorohitra iliyoko katika mji mkuu, Antananarivo, na kutangaza kuchukua uongozi wa nchi.

Kanali Randrianirina alisema: “Kwa kutumia Amri namba 2025-001, tumeamua kusitisha utekelezwaji wa katiba iliyopitishwa Desemba 11, 2010, na kuanzisha mifumo mipya kwa ajili ya mageuzi ya kitaifa.”

Aliongeza kuwa: “Kipindi cha mpito kitadumu kwa muda usiozidi miaka miwili. Katika kipindi hiki, kura ya maoni itafanyika ili kuunda katiba mpya, kisha uchaguzi utafanyika kuanzisha taasisi mpya hatua kwa hatua.”

Inayohusiana

Taasisi zilizosimamishwa

 Taasisi tano zimesimamishwa kazi, nazo ni: Mahakama ya Katiba ya Juu, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Seneti, Baraza Kuu la Ulinzi wa Haki za Binadamu, na Mahakama ya Juu ya Haki.

Hata hivyo, Bunge la Taifa limesalia kama taasisi pekee inayofanya kazi.

Jeshi lilitangaza kuwa nafasi ya urais sasa itashikiliwa kwa pamoja na maafisa wake wa kijeshi.

Mapema siku hiyo, Rajoelina alivunja bunge kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali kote nchini, akisema ni muhimu kurejesha utulivu na kutoa nafasi kwa vijana. Hata hivyo, bunge lilipiga kura na kupitisha hoja ya kumuondoa rais mahakamani.

Rajoelina asema yuko “mahali salama” 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *