Leo ni Jumanne tarehe 21 Mfunguo Saba Rabiul-Thani 1447 Hijria Qamaria, sawa na tarehe 22 Mehr mwaka 1404 Hijria Shamsia, inayosadifiana na tarehe 14 Oktoba 2025 Miladia.

Miaka 211 iliyopita katika siku kama ya leo, yaani Oktoba 14, 1814, mkutano wa kihistoria wa Vienna ulifanyika kwa lengo la kujadili  “Ulaya ya baada ya Napoleon Bonaparte”. 

Baada ya kujiuzulu na kubaidishwa Bonaparte mwezi Aprili mwaka 1814, mkutano wa kihistoria wa Vienna ulianza kufanyika katika siku kama ya leo katika mji mkuu huo wa Austria ili kuchukua maamuzi kuhusu ardhi zilizokaliwa kwa mabavu na Ufaransa katika kipindi cha vita vya Bonaparte.

Wakati wa kuendelea mkutano huo, Napoleone Bonaparte alikimbia kutoka mahala alipokuwa amebaidishiwa; na mwishoni mwa mwezi Februari mwaka 1815 kwa mara nyingine tena akashika hatamu za uongozi kwa muda mfupi, kipindi ambacho kiliondokea kuwa mashuhuri kwa jina la “Utawala wa Siku 100”.

Aliposhika tena hatamu za uongozi alijianda kuwashambulia maadui zake. 

Katika siku kama ya leo miaka 92 iliyopita, yaani tarehe 14 Oktoba, 1933, kwa amri ya Kansela wa wakati huo wa Ujerumani Adolf Hitler, nchi hiyo ilijitoa katika Shirikisho la Mataifa (The League of Nations).

Kuingia madarakani Hitler akiwa Kansela wa Ujerumani kulizusha wasiwasi mkubwa katika kila kona ya Ulaya kutokana na mipango yake ya kijeshi.

Baada ya kumalizika Vita vya Kwanza vya Dunia na kutiwa saini mkataba wa amani wa Warsaw ambao ulidhibiti sana zana za kijeshi za Ujerumani, Hitler na viongozi wengine wa Kinazi walikasirishwa mno na hatua hiyo. 

Miaka 75 iliyopita katika siku kama ya leo, yaani tarehe 21 Rabiu-Thani, 1371 Hijria Qamaria, aliaga dunia mwanachuoni mkubwa wa zama hizo, Ayatullah Muhammad Nahavandi. Ayatullah Muhammad Nahavandi, mwana wa mwanazuoni mchamungu Ayatullah Mirza Abdul Rahim Nahavandi, alizaliwa Najaful-Ashraf nchini Iraq. Kama alivyokuwa baba yake, Ayatullah Nahavandi anatambuliwa kuwa mmoja wa wasomi na wanazuoni wakubwa wa karne ya 14 kwa ubobezi wake katika elimu, matendo, na maadili. Miongoni mwa athari zilizoachwa na alimu huyo ni tafsir ya al-Mabsut ya Kiarabu na Kifarsi na mkusanyiko wa vitabu viwili katika juzuu 4, viitwavyo Nafahaatu-Rahman.

Ayatullah Muhammad Nahavandi

Siku kama ya leo miaka 71 iliyopita, Wazayuni wa Israel walivamia kijiji cha Qibya kilichoko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kufanya jinai kubwa za kutisha.

Katika mashambulizi na uvamizi huo ulioendelea katika kijiji hicho kwa muda wa siku mbili, Wazayuni walifanya mauaji na ukatili mkubwa dhidi ya raia wa Kipalestina wasio na hatia. Mbali na Wazayuni hao kuwaua na kuwajeruhi kwa umati raia wa Kipalestina zaidi ya 42, askari wa Israel waliokuwa wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon, walibomoa makumi ya nyumba na skuli za kijiji hicho.

Mauaji hayo ya halaiki ni miongoni mwa mifano ya ugaidi wa utawala ghasibu wa Israel hususan wa waziri mkuu wa zamani wa utawala huo, Ariel Sharon. 

Mandhari ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na Wazayuni katika kijiji cha Qibya

Na katika siku kama ya leo miaka 60 iliyopita, yaani tarehe 14 Oktoba mwaka 1964 Nikita Khrushchev, Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomonisti cha Umoja wa Sovieti aliuzuliwa wadhifa wake huo.

Khrushchev aliteuliwa kuwa mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Chama cha Kikomonisti mwaka 1939; na baada ya kufariki dunia Joseph Stalin mwaka 1953, alijitokeza kuwa shakhsia mwenye nguvu katika umoja wa Sovieti na kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomonisti na baadaye Waziri Mkuu wa shirikisho hilo. 

Nikita Khrushchev

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *