Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, limewahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa kuchagua viongozi bora na kuepuka vitendo vyote vinavyoweza kuharibu amani…likiwataka kuwa mabalozi wa amani na kutunza mshikamano wa kitaifa.

Hayo yalisemwa na Askofu Mteule wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Dkt. George Pindua, wakati wa matembezi ya amani ya kupanda Milima ya Uluguru, yaliyojihusisha na zaidi ya vijana 700 kutoka jimbo la Morogoro. Matembezi haya yalifanywa kama sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *