Katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 26 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Athumani Janguo amesimulia jinsi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyolianzisha shirika hilo mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema Nyerere alitambua reli kuwa uti wa mgongo wa maendeleo, akisisitiza umuhimu wa miundombinu ya usafiri kuunganisha Watanzania kutoka pwani hadi bara.
Kwa mujibu wa Janguo, uanzishwaji wa TRC ulikuwa sehemu ya falsafa ya kujitegemea kiuchumi na kujenga taifa lenye umoja na uzalendo.
Ameeleza kuwa utekelezaji wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge (SGR) ni mwendelezo wa ndoto ya Mwalimu Nyerere ya kujenga usafiri wa uhakika na wa kisasa unaochochea uchumi wa viwanda.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates