KUTOKA GYMKHANA: “Leo Yanga ni brand kubwa sio tu Tanzania, sio tu Afrika”

KUTOKA GYMKHANA: “Leo Yanga ni brand kubwa sio tu Tanzania, sio tu Afrika”
Mwanahabari mkongwe nchini Gerald Hando amesema tangu Hersi Said aingie katika madaraka katika klabu ya Yanga, chapa ya timu hiyo imekua kwa kiwango kikubwa.

Hando amekumbushia namna mambo yalivyokuwa hapo zamani na hasa kwenye mikutano ya Yanga, ambapo askari walikuwa wanahitajika kuimarisha ulinzi wa kiwango cha juu.

Ni kwenye tukio maalumu kumhusu Rais wa Yanga SC, Hersi Said.

Kwa sasa Hersi ni Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu Afrika (ACA) lakini pia hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya FIFA kwa ngazi ya klabu.

Tuko LIVE #AzamSports1HD

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#Yangasc #HersiSaid #Hersi #Yanga #IamHersi #ACA #FIFA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *