
Lecornu amechukua hatua hiyo kutokana na shinikizo alilowekewa na wabunge wa mrengo wa kushoto, waliokuwa wamemtaka achukue hatua hiyo ili aweze kusalimika kisiasa.
Waziri mkuu huyo anayekabiliwa na kibarua cha kunusurika kura mbili za maoni wiki hii, ametangaza hilo bungeni kama sehemu ya hatua ya mwisho ya kujaribu kuweka mazingira ya kupitisha bajeti ya mwaka 2026.
Ufaransa iko katika mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miongo kadhaa huku Lecornu akiwa waziri mkuu wa sita kuteuliwa na Rais Emmanuel Macron katika kipindi cha miaka miwili.