Adhieu Marial amesimama kwa kile kilichobaki kwa nyumba yake katika Jimbo la Unity la Sudan Kusini, akitathmini kilichobaki baada ya mafuriko.

“Kwanza, tumekimbia mashambulizi ya risasi. Sasa,tunakimbia maji,” mama huyo mwenye watoto wanne ameiambia TRT Afrika.

Katika wiki za hivi karibuni, mito iliyofurika imefunika sehemu kubwa ya majimbo ya Jonglei, Upper Nile na Unity, na kusababisha watu zaidi ya 100,000 kuachwa bila makazi yao. Wengi wao walikuwa ndiyo wanaanza tu kujenga upya maisha yao baada ya kulazimika kukimbia mapigano yaliyotibuka mapema mwaka huu.

Sasa, mafuriko yana watatiza tena.

Adhieu, ni miongoni mwa wale wanaojaribu kuweka sawa maisha yao huku wakikabiliana na janga lingine, ameamua kuangazia mustakabali wake.

“Mafuriko yalifunika nyumba yetu, lakini bado tuna matumaini. Kwa mabati haya tuliyopata kutoka kwa mashirika ya misaada, angalau tumepata sehemu ya kujistiri. Watoto wangu wako salama kwa sasa,” anasema Adhieu, akiwa anawakilisha hisia za maelfu ya watu.

Matatizo mbalimbali

Kila siku, kuna matumaini kwa wale waliopoteza makazi yao Sudan Kusini.

Shirika linaloshughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeonya kuwa kama mafuriko yataendelea, watu hadi ya 400,000 watakuwa wamepoteza makazi yao kufikia mwisho wa mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *