Manchester, England. Shabiki wa damu kabisa wa mchezo wa soka aliyebadili jina lake na kuitwa Mr Manchester United na kuchora tattoo ya nembo ya klabu hiyo kwenye paji lake la uso amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Marin Zdravkov Lavidzhov, aliyekuwa mfanyakazi wa ujenzi huko Bulgaria, alianza kuipata Man United baada ya tukio la kupindua meza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich uwanjani Nou Camp mwaka 1999.

Baada ya hapo alipambana kwenye kesi mahakamani kwa miaka 15 ili kupata haki ya kubadili jina lake na kuitwa Manchester United, kesi ambayo aliibuka mshindi 2014.

M 01

Huko nyumbani kwake Bulgaria kumepambwa na vitu mbalimbali vya Man United, ikiwamo jezi, mabango, skafu na picha za wachezaji wake vipenzi, akiwamo Mbulgaria, Dimitar Berbatov.

Lakini, kwa masikitiko makubwa, shabiki huyo ambaye jina lake lilibadilika na kuitwa Manchester Zdravkov Levidzhov-United amefariki dunia.

Mr United baada ya ushindi ule wa 2-1, Man United iliopata mabao yake kwenye dakika za majeruhi dhidi ya Bayern, kwa furaha tangu siku hiyo aliamua kubadili jina, jambo lililomhitaji kupata nguvu ya kisheria. Vita yake ya kupambana mahakamani kubadili jina ilitengenezewa filamu maalumu huko Bulgaria mwaka 2011 iliyofahamika My Mate Manchester United.

M 02

Baada ya muongo mmoja na nusu wa kushinda vita hiyo ya kisheria, shabiki huyo alisherehekea ushindi wake kwa kuchora tattoo ya beji ya Man United kwenye paji la uso wake.

Mwaka 2014, gazeti la The Sun lilitimiza ndoto zake za kumfanya atembelee Old Trafford. Mr United alipewa nafasi ya kufanya ziara maalumu ya kutembelea Theatre of Dreams kabla ya kwenda Stadium of Light kwenda kushuhudia Man United ikikipiga na Sunderland.

M 03

Mr United amesema: “Nitaikumbuka siku hii maisha yangu yote na nitakwenda kuiambia familia yangu na marafiki zangu kuhusu hii kitu kwa muda wote wa uhai wangu.”

Mr United, ambaye paka wake alimpa jina la David Beckham kutokana na kuwa na mapenzi makubwa kwa mchezaji huyo alisafiri umbali wa maili 4,000 kwa ajili ya ziara hiyo. Na alijikuta akiangua kilio baada ya kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia vya wachezaji na machozi yalimtoka pia alipoingia kwenye nyasi za uwanja wa Old Trafford.

M 04

Mr United alirudi tena Manchester mwaka 2017 kwenye kipindi cha pre-season. Hakuna mengi yanayofahamika kuhusu maisha yake mengine, lakini kikubwa ni ushabiki wake kwa Man United ambao umeacha alama unaokumbukwa miaka yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *