Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime amesema hali ya ulinzi na usalama nchini kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 imeendelea kuwa shwari, huku likiendelea kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali wa usalama kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
Aidha, DCP Misime ameeleza kuwa kumekuwa na kupungua kwa matukio ya kihalifu kama vile ukabaji, uporaji na uvamizi wa majumbani, hali inayoashiria ufanisi wa juhudi za jeshi hilo katika kudhibiti uhalifu na kulinda mali pamoja na maisha ya wananchi.
#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri| John Mbalamwezi