Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime amewahakikishia wananchi kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha amani na usalama wakati wa uchaguzi mkuu. Amesema wananchi wanapaswa kwenda kupiga kura bila hofu kwani kila hatua ya mchakato imetiliwa mkazo katika kulinda usalama wao.
Aidha, DCP Misime amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi kuhakikisha uchaguzi unaisha kwa amani, utulivu na bila matukio ya uvunjifu wa sheria.
#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri| John Mbalamwezi