Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili, 1922 katika kijiji cha Butiama, mkoani Mara

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13 Aprili, 1922 katika kijiji cha Butiama, mkoani Mara. Alikuwa mtoto wa chifu Nyerere Burito wa kabila la Wazanaki. Baada ya elimu ya msingi na sekondari, alisoma Makerere (Uganda), kisha kuendelea na masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uingereza — akiwa Mtanganyika wa kwanza kupata shahada ya juu katika chuo hicho.

Baada ya kurejea nchini, alifanya kazi kama mwalimu na baadaye kuanzisha chama cha TANU (Tanganyika African National Union) mwaka 1954, ambacho kiliongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Kupitia uongozi wake wa busara, Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, na baadaye kuungana na Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964.

Akitumikia kama Rais wa Kwanza wa Tanzania, Nyerere alijulikana kwa siasa za Ujamaa na Kujitegemea, akisisitiza umoja, elimu na usawa wa kijamii. Alistaafu kwa hiari mwaka 1985 lakini aliendelea kuwa mshauri muhimu kitaifa na kimataifa.

Mwalimu Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba 1999 jijini London. Leo, tunatimiza miaka 26 bila Baba wa Taifa, lakini fikra, maadili na urithi wake vinaendelea kuiongoza Tanzania.

#StaeTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *