Rais wa Madagascar Andry Rajoelina siku ya Jumanne alivunja bunge, na hiyvo kupindua azma ya bunge kumuondoa madarakani, iliyoongozwa na upinzani, kutokana na mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Rajoelina amekabiliwa na zaidi ya wiki mbili za maandamano barabarani, yakiongozwa kwa kiasi kikubwa na waandamanaji vijana, na kumlazimisha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 51 kujificha.
Agizo la kuvunja bunge “litaanza kutekelezwa mara moja baada ya kutangazwa kwenye redio na/au matangazo ya televisheni”, ilisema taarifa ya rais katika ujumbe uliyowekwa kwenye Facebook.
Rajoelina, ambaye amekaidi wito unaoongezeka wa kumtaka ajiuzulu, alitetea hatua hiyo katika ujumbe tofauti kwenye mtandao wa kijamii kama muhimu “kurejesha utulivu ndani ya taifa letu na kuimarisha demokrasia.”
“Lazima watu wasikike tena. Vijana wapewe nafasi,” alisema kupitia mtandao wa kijamii.