Rais huyo ametangaza hayo kupitia taarifa aliyoichapisha kwenye ukurasawa mtandao wa kijamii wa Facebook Jumanne.

Lakini kiongozi wa upinzani bungeni amesema kuwa hajashauriwa kuhusiana na amri ya rais ya kulivunja bunge.

Tangazo la Rajoelina limetolewa katika wakati Jeshi la polisi la Madagascar limeungana na maandamano yanayoongozwa na vijana ya kumpinga kiongozi huyo.

Haya ni kulingana na shirika moja la habari nchini humo. Mkuu wa polisi ameongeza kuwa inashikamana na jeshi akisisitiza uungwaji mkono mkubwa wa kitaasisi kwa maandamano hayo.

Rais Rajoelina aliikimbia Madagascar Jumapili kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Ufaransa.

Rais huyo alisema kwamba amekimbia ili kuyalinda maisha yake.

Rajoelina ambaye alipata uraia wa Ufaransa mwaka 2014, hajatangaza alipo kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *