Baada ya siku nne chini ya ulinzi wa polisi, hatimaye kaka wa rais wa zamani wa Senegal, Macky Sall, na mkewe waachiliwa. Aliou Sall na mkewe ambao wamekuwa wakishukiwa kuwa nyuma ya shughuli ya mali isiyohamishika na idara ya kupambana na ufisadi nchini Senegal, wameachiliwa kwa dhamana ya faranga za CFA milioni 240. Hata hivyo, walishtakiwa kwa “utakatishaji fedha” na “njama ya uhalifu.” 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Baada ya siku nne chini ya ulinzi wa polisi, Aliou Sall, kaka wa rais wa zamani wa Senegal Macky Sall na meya wa zamani wa vilaya ya Guediawaye, na mkewe wameachiliwa siku ya Jumatatu, Oktoba 13 kwa dhamana ya faranga za CFA milioni 240 (zaidi ya euro 365,000).

Kama sehemu ya uchunguzi uliofunguliwa na kitengo cha Mahakama ya Kifedha ya Senegal (PJF), wote wawili walishtakiwa kwa “utakatishaji fedha” na “njama ya uhalifu” kufuatia shughuli ya mali isiyohamishika iliyoonekana kutiliwa shaka, yaani, ununuzi wa shamba la mita za mraba 1,000 karibu na Ubalozi wa Marekani katika kitongoji cha Almadies huko Dakar.

Uhamisho na malipo ya benki yanayotiliwa shaka

Sababu: kununuliwa kwa kampuni ya mali isiyohamishika ya Aliou na Aïssata Sall, ambayo haikukosa kuvutia umakini wa idara ya kupambana na ufisadi wa Senegal.

Kulingana na wakili wa kaka ya Macky Sall na mkewe, malipo kadhaa na uhamisho wa benki wa jumla ya faranga za CFA milioni 240 umeibua mashaka ya Kitengo cha Kitaifa kinachohughulikia Taarifa za Fedha (CENTIF), ambacho kinabaini kuwa miamala hii inaweza kuwa utakatishaji fedha.

Aliou Sall, kwa upande wake, anahakikisha kuwa ununuzi wa ardhi husika ulifadhiliwa na mkopo wa benki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *