Serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) inaendelea kutekeleza miradi 13 ya dharura ya ujenzi wa barabara na madaraja mkoani Lindi kwa gharama ya shilingi bilioni 119, ili kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na mvua za El-Nino na kimbunga Hidaya.

Msimamizi wa miradi ya maendeleo TANROADS mkoa wa Lindi, Mhandisi Fred Sanga amesema zaidi ya shilingi bilioni 58.5 zimeshalipwa kwa wakandarasi na kazi inatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

Ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetenga shilingi bilioni 16.2 kwa miradi ya matengenezo na maendeleo ikiwemo ujenzi wa zaidi ya kilomita 1,300 za barabara na madaraja matatu katika barabara za Kilwa Masoko–Liwale, Matangini–Chiola–Likunja, na Chiola–Ruponda.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *