.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United na Crystal Palace wanamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Muingereza Jobe Bellingham, 20. (Bild – in Germany, Subacsription Required)

Arsenal, Manchester City na Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Ujerumani Nathaniel Brown mwenye umri wa miaka 22 kutoka Eintracht Frankfurt, lakini klabu hiyo ya Bundesliga haitasikiliza ofa hadi msimu ujao wa joto. (Bild – in Germany)

Iwapo Eintracht Frankfurt itamruhusu Brown – ambaye hana kipengele cha kutolewa katika mkataba wake – kuhama, klabu hiyo ya Ujerumani itadai pauni milioni 52. (Florian Plettenberg)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Msako wa Chelsea kumnasa Adam Wharton wa Crystal Palace umeongezeka lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United kumnunua kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 21. (Teamtalks)

Mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz, 21, anatazamiwa kukataa nia ya Arsenal, Chelsea na Manchester United ili kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Juventus. (Tuttosport – In Itali)

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Ujerumani na Bayern Munich Aleksandar Pavlovic, 21. (Football Insider).

Real Madrid wanafikiria kwa dhati kumuuza winga wa Brazil Vinicius Junior, 25, katika klabu moja nchini Saudi Arabia. (Sky Sports – In French)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Watford wanatafuta dili la kumnunua mshambuliaji Emmanuel Dennis kufuatia kuachiliwa kwake na Nottingham Forest mwezi Agosti, huku West Ham pia wakimtaka Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 27. (Mail)

Paris St-Germain wameambiwa watalazimika kulipa pauni milioni 52 kumnunua kiungo wa kati wa Roma Mfaransa Manu Kone, 24. (Corriere dello Sport – In Italy),

Wakala wa mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski ametilia shaka mustakabali wa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 37 katika klabu hiyo, huku kandarasi yake ikitarajiwa kuisha msimu ujao wa joto na hakuna ofa mpya inayokuja. (Sport – In Spanish)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *