.

Chanzo cha picha, Reuters

Rais wa
Madagascar Andry Rajoelina amesema “nimejificha mahali salama” baada
ya jaribio la kumuua, kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya kumtaka ajiuzulu.

Katika
matangazo ya moja kwa moja kwa taifa kupitia ukurasa wa Facebook, Rajoelina,
51, alisema “kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua”.

Hakufichua
eneo aliko, lakini ripoti ambazo hazijathibitishwa awali zilidokeza kwamba
alitoroka nchini kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.

Hilo limetokea
baada ya maandamano ya nchi nzima, hasa yakiongozwa na vijana, yenye lengo la
kumuondoa madarakani.

Jaribio
lililofeli la Rajoelina kuwatuliza waandamanaji hao vijana – walioitwa “Gen Z Mada” – lilimshuhudia rais akiifuta kazi serikali yake yote na
kufanya makubaliano mengine bila mafanikio.

Hajaonekana
tangu Jumatano, na mwishoni mwa wiki ofisi ya Rajoelina ilisema jaribio
lilikuwa linaendelea kumlazimisha kuondoka madarakani.

Hotuba yake
kwa taifa ilicheleweshwa mara kadhaa Jumatatu huku kukiwa na machafuko, wanajeshi
nao wakitishia kuteka makao makuu ya Televisheni ya taifa katika kisiwa cha
Bahari ya Hindi.

Hatimaye,
katika matangazo ya Facebook alisema: “Tangu Septemba 25, kumekuwa na
majaribio ya kuniua na ya kufanya mapinduzi. Kundi la wanajeshi na wanasiasa
walipanga kuniua.

“Nililazimika
kutafuta mahali salama ili kulinda maisha yangu.”

“Kuna
njia moja tu ya kutatua masuala haya; ambayo ni kuheshimu katiba inayotumika
nchini”.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *