Ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 pamoja na barabara unganishi na mchepuko zenye jumla ya kilomita 25 umefikia asilimia 74.3 hadi kufikia Septemba 30, 2025. Kukamilika kwa daraja hilo kutarahisisha usafiri, kuongeza fursa za biashara, kuchochea utalii na kuimarisha uchumi wa buluu.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Tanga, Mhandisi Msama Msama, amesema kuwa kazi zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa kuta unganishi mbili na nguzo nane za kati, huku zaidi ya shilingi bilioni 45.6 zikiwa zimeshalipwa kwa mkandarasi CHICO kutoka China.
Mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unalenga kuimarisha miundombinu ya usafiri na kuunganisha Mkoa wa Tanga na ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki kupitia njia ya Malindi, Mombasa, Horohoro, Tanga, Pangani, Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 454.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi