Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu  Christian Cardon amefafanuwa dhamira ya  mashirika hayo ya kutaka kuingiza misaada kwa wingi katika ukanda huo wa Gaza.

“Ndio usalama unastahili kuzingatiwa, ila ni pale malori yatakapoingiaUkanda wa Gaza. Ila kabla hapo, kuna hizo njia zakuingia. Kulingana na ninavyojua mimi, si njia zote ziko wazi kwa ajili ya misaada kuingia Gaza na hilo ndilo tatizo kuu kwa sasa. Na hilo ndilo ambalo mashirika ya misaada yamekuwa yakitaka lifanyike, njia zote zifunguliwe kwasababu ya mahitaji makubwa yaliyopo,” alisema Cardon.

Haya yanafanyika wakati ambapo mamlaka  Palestinazinasema sehemu ya kwanza ya miili ya Wapalestina waliouwawa wakati wa vita hivyo vya Gaza, imewasili katika mamlaka hiyo leo baada ya kuachiwa na Israel. Israel bado inaishikilia mamia ya miili ya Wapalestina waliouwawa tangu shambulizi la Oktoba 7 mwaka 2023 wakiwemo wapiganaji walioshirika uvamizi huo na waliopigana baada ya hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *