.

Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema ushirikiano wa kijeshi na Iran utaendelea “kwa mujibu wa sheria za kimataifa,” hata baada ya vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa vilivyoondolewa baada ya JCPOA kurejeshwa Septemba 27. Urusi haitambui vikwazo hivyo.

“Hakuna vikwazo kwa ushirikiano wetu wa kijeshi na kiufundi na Iran baada ya kuondolewa vikwazo vya Umoja wa Mataifa, kwa hivyo tunatoa vifaa ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inavihitaji kwa kufuata kikamilifu sheria za kimataifa. Nasisitiza tena kwamba hilo linafanyika kwa kufuata kikamilifu sheria za kimataifa,” Bw Lavrov aliambia Reuters.

Marufuku ya silaha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilimalizika Oktoba 2020. Chini yake, Iran haikuwa na vikwazo vya kisheria vya kununua na kuuza silaha, lakini Baraza la Usalama lilipiga kura ya kurejesha maazimio haya na vikwazo vinavyohusiana. Marekani iliunga mkono, huku China na Urusi zikipinga kurejeshwa kwa vikwazo hivyo.

Nchi tatu za Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, kwa kuzingatia mamlaka ya Azimio la 2231, zilifungua njia ya kurejeshwa kwa vikwazo hivi, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya silaha.

.

Chanzo cha picha, AFP

‘Tunatumai ushirikiano wetu wa Urusi na China hautaathiriwa’

Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na ripoti katika vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu usafirishaji wa zana nzito za kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege za kijeshi za Urusi, hadi Iran. Iran na Urusi hazijathibitisha wala kukanusha ripoti hizi.

Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema tarehe 13 Oktoba kuhusiana na uamuzi wa Baraza la Usalama la kurudisha maazimio hayo na kutekeleza upya vikwazo hivyo: “Tunaendelea na mashauriano kati ya China na Urusi na tuna imani kuwa uhusiano wetu na nchi hizi mbili katika maeneo mbalimbali hautaathiriwa na matukio hayo.”

Akirejelea upinzani wa Urusi na China wa kuirejeshea vikwazo Iran, Bwana Baghaei alisema: “Lau wasingeliamini jambo hili, wasingekuwa na msimamo huo wa wazi. Msimamo wao wa umma na uliothibitishwa kisheria kwa kuzingatia ushahidi wa kisheria utaonyesha athari zake za kisheria katika suala la kuendeleza uhusiano wa Iran na nchi hizi mbili.”

Serikali ya Iran imezitaka nchi duniani kote kutotekeleza tena maazimio ya Baraza la Usalama na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Katika barua, wameutaka Umoja wa Mataifa kukomesha vizuizi vyote vinavyohusiana na azimio nambari 2231 katika tarehe ya mwisho ya Oktoba 18.

Hata hivyo, kwa uanzishaji wa utaratibu wa trigger na kurudi kwa vikwazo, tarehe hii imepitwa na wakati, lakini Iran inatambua.

Baada ya kufufua maazimio hayo, Umoja wa Mataifa umeziarifu nchi wanachama juu ya utekelezaji wake upya katika taarifa rasmi.

.

Chanzo cha picha, EPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *