Wataalum wa Mazingira kutoka nchini Finland wanawajengea uwezo wakufunzi kutoka Chuo Cha Viwanda vya Misitu (FITI) na Chuo Cha Misitu Olmotonyi pamoja na Chuo Cha Misitu Zambia juu ya maendeleo endelevu ya Misitu na Mazao yake.
Moja ya faida ya kujengewa uwezo huo ni pamoja na kuwezesha wakufunzi hao kutoa Elimu inayoendana na Hitaji la Soko la Ajira ya kuajiriwa au kujiajiri linaloenda sambamba na ukuaji wa Sayansi ya Technolojia.
Warsha hiyo ya kujengewa uwezo inafanyika Mkoani Kilimanjaro katika Chuo Cha Viwanda vya Misitu FITI.
#StarTvUpdate