Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameahidi kujenga uwanja mkubwa wa ndege katika eneo la Kyabajwa, Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, endapo atachaguliwa kuunda serikali baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Amesema uwanja huo utahudumia ndege kubwa ikiwemo Boeing 737, na kufungua fursa za utalii, biashara na kilimo biashara kwa wananchi wa Kagera na maeneo ya mpakani mwa Uganda.

Amefafanua kuwa upembuzi yakinifu wa mradi huo umekamilika, na ujenzi wake utasaidia kusukuma mbele juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu ya usafiri na ukuaji wa uchumi wa kanda ya ziwa.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *