Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumanne, Oktoba 14, kwamba uungaji mkono wake kwa Argentina “kwa namna fulani” utatokana na matokeo ya uchaguzi ujao wa wabunge, ambao utakuwa wa maamuzi kwa muda uliosalia wa mshirika wake, Rais wa Argentina Javier Milei.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Uungwaji mkono wetu kwa namna fulani unafungamana na nani atashinda uchaguzi,” rais wa Marekani amesema wakati akimkaribisha Javier Milei kwenye Ikulu ya White House, akihakikisha kwamba katika tukio la ushindi wa “wasoshalisti,” “tunafikiri kwa namna tofauti kuhusu uwekezaji tunaofanya.”

Rais wa Argentina mwenye msimamo mkali Javier Milei alipokelewa katika Ikulu ya White House na mshirika wake wa kiitikadi Donald Trump ili kusahihisha msaada wa kifedha uliotangazwa hivi karibuni na Washington, wiki mbili kabla ya uchaguzi muhimu kwa muda uliosalia wa muhula wake.

Miiko inavunjika moja baada ya nyingine. Wakati huu, Donald Trump anamfanyia kampeni Javier Milei mbele ya waandishi wa habari, akitoa mfano wa ukaribu wa kiitikadi kati ya wawili, hao anaripoti mwandishi wetu wa Washington, Vincent Souriau.

“Iwapo rais wa sasa hatashinda, najua mpinzani wake atakuwa nani. Yeye ni mtu wa mrengo wa kushoto mno na falsafa ambayo imeiongoza Argentina kwenye matatizo inayoikabili kwa sasa,” rais huyo wa Marekani amesema.

“Tunataka tu afanikiwe”

Donald Trump anajua vyema kuwa uchaguzi unakaribia. Huu sio uchaguzi wa rais; ni uchaguzi wa wabunge ulioratibiwa kwa zaidi ya siku kumi nchini Argentina, unaochukuliwa kuwa muhimu na Javier Milei. Na kama njia ya kutoa shinikizo kwa wapiga kura wa Argentina, Donald Trump anatishia kusitisha msaada wa kifedha katika tukio la mabadiliko ya kisiasa.

“Anaweza kushinda, anaweza asishinde. Nadhani atashinda… Ikiwa atashinda, tutabaki nao. Ikiwa hatashinda, tutaondoka,” anaonya Donald Trump. Argentina ni “mojawapo ya nchi nzuri sana ambazo nimewahi kuona,” anahitimisha Donald Trump. “Ni rahisi sana, tunataka tu afanikiwe.”

Javier Milei anaishukuru Marekani kwa msaada wake wa peso

Hazina ya Marekani ilitangaza Alhamisi, Oktoba 9, kubadilishana kwa sarafu ya nchi mbili ya dola bilioni 20 na kuingilia moja kwa moja katika soko la fedha za kigeni ili kusaidia sarafu ya Argentina (peso). Wakati wa mkutano na Donald Trump na wajumbe wa serikali yake, Javier Milei amemshukuru Waziri wa Fedha Scott Bessent kwa “kazi kubwa” ambayo amefanya kusaidia Argentina “kuondokana na tatizo la ukwasi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *