
Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumanne kuwa Marekai “itawapokonya silaha” Hamas ikiwa hawatoweka chini silaha. Katika Ukanda wa Gaza ulioharibiwa, Hamasinaendesha kampeni ya ukandamizaji na imetoa video ya watu wanaume wanane walioitwa “washiriki” na Israeli wakiuawa hadharani. Miili ingine minne ya mateka ilirejeshwa Israel usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Ikiwa hawasalimisha silaha zao wenyewe, tutawapokonya silaha,” Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Jumanne, Oktoba 14, kuhusu Hamas. “Itatokea haraka na labda kwa vurugu,” amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, bila kutoa maelezo zaidi juu ya namna operesheni hiyo ya upokonyaji silaha itafanyika, wala makataa aliyotoakwa kundi la wanamgambo wa Hamas.
Hamas ilipanua uwepo wake katika Ukanda ulioharibiwa wa Gaza siku ya Jumanne, Oktoba 14, ikiendesha ukandamizaji na kuwaua “washirika” wanaoshukiwa wa srael, wakati ambapo Donald Trump alipokuwa akisema kuwa Washington itawapokonya silaha Hamas ikiwa watasita kusalimisha silaha zao.
Rais wa Marekani pia aliitaka Hamas kurudisha mabaki ya mateka waliofariki huko Gaza, hatua ambayo anaona ni muhimu kuelekea katika awamu inayofuata ya mpango wake wa ardhi ya Palestina iliyoharibiwa na vita vya miaka miwili.
Hamas ilikabidhi miili mingine minne kwa Shirika la Msalaba Mwekundu Jumanne jioni, jeshi la Israel limesema, ambalo lilipokea majeneza muda mfupi baada ya saa sita usiku Jumatano.
Siku ya Jumatatu, iliwaachilia mateka hai 20 wa mwisho iliyokuwa ikiwashikilia tangu shambulio lililoanzisha vita mnamo Oktoba 7, 2023, badala ya karibu wafungwa 2,000 walioachiliwa na Israel, na kukabidhi mabaki ya mateka wanne. Kwa upande wake, Israel ilikabidhi mabaki ya Wapalestina 45, waliopelekwa katika Hospitali ya Nasser iliyoko Khan Younis (kusini).