#HABARI: Kesi ya jinai namba 25480 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili (Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu) dhidi ya viongozi waandamizi wa chama hicho wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche imetajwa leo Mahakamani hapo chini ya Jaji Awamu Mbagwa.

Leo Mahakamani hapo, upande wa mashtaka umewasilishwa flash ambayo ina picha jongefu (video) zinazoonesha kauli zilizotolewa kwa nyakati tofauti kupitia majukwaa tofauti, kauli ambazo zinadaiwa kukiuka amri ya Mahakama ya Juni 10.2025.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Oktoba 22, 2025 kwa kile kilichoelezwa na Mahakama kuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura, ambapo pia waleta maombi wametakiwa kuwapatia taarifa baadhi ya watuhumiwa ambao hawajawafikishia taarifa hiyo haraka iwezekanavyo.

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *