#HABARI: Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kalambo mkoani Rukwa Ndugu Edifonce Kanoni, amesema andapo akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo, atahakikisha anamalizia ujenzi wa masoko yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi, hatua itakayosaidia wajasiriamali wadogo kuimarika kiuchumi.
Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi kupitia mkutano wa kampeni uliofanyika katika vijiji vya Kamawe,Ilambila na Kalaela kata ya Sundu wilayani humo, na kusema ataishauri serikali kukamilisha ujenzi wa shule ya Sekondari Sundu ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya shule za msingi kwa kuweka viti na meza.
Pamoja na mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi, kujikita kwenye kilimo chenye tija, ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kuuza ardhi kiholela.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania