#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Albert Chalamila, amekagua miradi ya ujenzi wa madaraja na barabara Jijini Dar es Salaam yenye gharama ya shilingi Bilioni 224.22 inayotekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kumlaki Chalamila amemtaka wakandarasi kuhakikisha anakamilisha miradi hiyo haraka iwezekanavyo na kwa muda uliopangwa.
RC Chalamila ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 pamoja na barabara unganishi (0.7km), linalojengwa na Mkandarasi M/s China Communications Construction Company Ltd kwa ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendeshaji wa Bonde la Msimbazi huku Mhandisi Mshauri ni M/s Leporogo Specialist Engineers ya Afrika Kusin iikishirikiana na Afrisa Co nsulting Ltd ya Tanzania na Dong Myeong Engineering Consultants &Architecture Co. Ltd ya Korea Kusini kwa gharama ya shilingi Bilioni 97.
Chalamila amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za kuwalipa wakandarasi ili kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba na kubainisha kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutarahisisha huduma za wananchi kwani watanzania wanasubiri kwa hamu na shauku kubwa miradi hiyo pindi itakapokamilika kwani itakuwa kichocheo cha maendeleo ya mkoa na kuepusha vifo visivyo vya lazima.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.