#HABARI: Rais Donald Trump amesema, Marekani imeishambulia boti nyingine kwenye pwani ya Venezuela na kuua watu sita, katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii, Trump amesema boti hiyo ni ya magaidi na ilikuwa ikisafirisha mihadarati.

Hili ni shambulio la tano la utawala wa Trump kwenye boti inayotuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kwenye maji ya Kimataifa tangu Septemba.

Jumla ya watu 27 wameripotiwa kuuawa, lakini Marekani haijatoa ushahidi au maelezo kuhusu utambulisho wa boti hizo au wale waliokuwemo.

Baadhi ya mawakili wameishutumu Marekani kwa kukiuka sheria za Kimataifa, na mataifa jirani kama Colombia na Venezuela yamelaani shambulio hilo.

Katika chapisho lake, Trump amesema “taarifa za kijasusi zimethibitisha kuwa boti hiyo ilikuwa ikisafirisha mihadarati, na inahusishwa na mitandao haramu ya wagaidi wa mihadarati, na ilikuwa ikipitia katika njia inayojulikana” kwa magendo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *