#HABARI:Wanufaika wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) mkoani Tabora wametakiwa kutumia fedha za ruzuku walizopewa kwa kufuata masharti ili kuhakikisha malengo ya kuboresha maisha ya wananchi na kuhifadhi misitu yanafikiwa.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TaFF, Dkt. Tuli Msuya, ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa vikundi zaidi ya 10 vya wafugaji nyuki vilivyonufaika na ruzuku kutoka mfuko huo.

Amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka 14 ya uendeshaji wake, TaFF imetumia Sh. bilioni 57.5 kugharamia miradi 1,245 nchi nzima, ambapo kati ya hizo, Sh. bilioni 3.1 zimetumika kutekeleza miradi 74 katika wilaya saba za Mkoa wa Tabora.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka TaFF, John Malemo, amewataka wanufaika kuhakikisha wanaandaa na kuwasilisha taarifa za matumizi ya fedha kwa wakati ili kurahisisha utoaji wa fedha za awamu zinazofuata, akisisitiza kuwa uwazi na uwajibikaji ndio msingi wa uendelevu wa ruzuku hizo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TaFF kwa kuwajengea uwezo, wakiahidi kutumia mafunzo hayo kuboresha shughuli za ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali, hatua ambayo wamesema itasaidia kuufanya Mkoa wa Tabora kuwa kinara wa uzalishaji wa asali nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *