Hatimaye Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dodoma, imeyeyusha ndoto ya urais ya kada wa Chama Cha ACT- Wazaleendo, Luhaga Mpina baada ya kuitupa kesi yake.
Kwa uamuzi huo, Mpina sasa hatoweza tena kushiriki katika mbio za Uchaguzi Mkuu ambako sasa vyama viko katika hatua za mwisho za kampeni kunadi sera zao zikiwa zimebaki siku 14 pekee.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano, Oktoba 15, 2025 kwa kile kilichoelezwa kuwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), haupaswi kuingiliwa na chombo chochote kwa jambo ambalo lilifanya kwa njia njema.
Kada huyo ambaye awali alitangaza kukihama Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), baada ya jina lake kukatwa katika kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera yake katika Jimbo la alifungua kesi mahakamani hapo akipinga kuenguliwa katika nafasi ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Uamuzi huo umetolewa mbele ya mahakama hiyo na kiongozi wa jopo la majaji wanasikiliza kesi hiyo, Jaji Fredrick Manyandam Majaji wengine waliosikiliza kesi hiyo ni Abdallah Gonzi na Sylvester Kainda.
#StarTvUpdate