
Katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara Ebimpé Olympic Stadium, Ivory Coast waliizidi maarifa Harambee Stars katika kila idara uwanjani.
Kwa ushindi huo, Ivory Coast imemaliza kileleni mwa Kundi F wakiwa na pointi 26, huku Kenya ikishindwa kufuzu baada ya kushikilia nafasi ya nne.
Kiungo Franck Kessié alifungua ukurasa wa mabao kunako katika dakika ya saba ya mchezo, akifuatiwa na Yan Diomandé aliyefunga la pili dakika ya 54, kabla ya Amad Diallo kufunga la tatu dakika ya 84.
Harambee Stars ya Kenya ilikuwa tayari imeondolewa kwenye mbio za kufuzu, na mechi hiyo ilikuwa ya heshima.
Kocha wa Kenya Benni McCarthy alijaribu mbinu ya kujilinda kwa safu ya nyuma ya wachezaji watano, lakini mfumo huo haukuweza kuzuia mashambulizi ya vijana wa Ivory Coast.