.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Vyombo vya habari vimeangazia kile kilichochukuliwa kuwa “siku ya kihistoria” kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka 20 waliosalia wa Israel waliokuwa wanashikiliwa na Hamas huku miili ya mateka waliofariki ikiendelea kurejeshwa.

Tuanze kwa kuangazia yaliokuwepo kwenye gazeti la The Independent, ambalo tahariri yake iliitwa “Ziara ya Ushindi ya Trump, na Mwanzo wa Mwisho wa Netanyahu.”

Gazeti hilo lilisema kwamba “tukio muhimu zaidi la siku ya kihistoria” lilikuwa kuachiliwa kwa mateka, sio hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa bunge la Israeli (Knesset) au “utendaji wa kuhadaa” wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Hata hivyo, gazeti hilo lilisema kwamba kutaja ukweli huu “hakupunguzi” juhudi za kidiplomasia za Trump, ambazo zilikuwa “sababu muhimu” katika kufikia usitishaji vita, kuachiliwa kwa mateka, kubadilishana kwa wafungwa wa Kipalestina, na matumaini ya kupatikana kwa amani ya kudumu, lilisema.

Gazeti hilo liliongeza, “Rais wa Marekani ana haki ya kile ambacho kimeelezewa na wengi kama mzunguko wa ushindi, lakini pia inahitaji mtazamo wa usawa wa kile kinachoweza kuzingatiwa kuwa siku ya kwanza ya mwanzo wa mwisho wa mzozo wa miongo kadhaa.”

Tahariri iliendelea: “Vita hivi vingeweza kumalizika kwa urahisi zaidi ya mwaka mmoja uliopita ikiwa Netanyahu angetaka, na kama Joe Biden (Rais wa zamani wa Marekani) angemlazimisha kuvimaliza.”

Kwa mtazamo wa hili, gazeti hilo lilisema, “Biden amekuwa akisisitiza kila mara uungaji mkono wake kwa Israel na amekuwa makini kuhusu hilo, huku uungwaji mkono wa Trump kwa Israel ukiegemea zaidi matakwa ya Marekani.

Kuhusu Netanyahu, gazeti hilo lilisema “haikuwa nia yake, na wala si mipangilio yake, kuishia na anayedhaniwa kuwa mshirika wake Trump kuzindua mpango unaolenga suluhu ya mataifa mawili na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.”

“Hakuna anayepaswa kushukuru” kwa Netanyahu, iliongeza.

Liliendelea: “Kwa madhumuni yake binafsi ya kisiasa, na kuepuka kurejea katika mahakama ya Israel kujibu mashtaka ya rushwa, ilikuwa rahisi kwa Netanyahu kuendeleza vita dhidi ya Hamas kwa muda usiojulikana – ingawa kwa hakika ilijumuisha ulipuaji wa mabomu na njaa kwa raia wa Palestina.”

Gazeti hilo lilisema, “Mpango wa amani uliowekwa na Trump kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya hatua mbaya za Netanyahu.”

Aliongeza, “Israel imetengwa kidiplomasia, na mwenendo wake katika vita umekuwa usiovumilika kwa mataifa ya Ghuba, kiasi kwamba rais wa Marekani hakuwa na chaguo ila kumtaka kiongozi huyo wa Israel kukoma.”

Mpango wa amani wa Trump “unalenga kutambuliwa majirani wote wa Israel kupitia upanuzi wa Mkataba wa Abraham, suluhisho la wazi la serikali mbili kwa suala la Israel na Palestina, na ujenzi wa Gaza,” kulingana na gazeti hilo.

Hata hivyo, alibainisha kuwa juhudi za awali za kufikia amani katika Mashariki ya Kati “zilikufa njiani baada ya kuanza kwa ahadi,” na kusema kwamba mpango wa Trump unaweza kuwa “uongo mwingine,” kwani “bado kuna mengi ya kuafikiwa, na suala la kuwapokonya silaha Hamas ni moja ya masuala muhimu ambayo bado yanahitaji kutatuliwa.”

Soma zaidi:

Kutafuta amani na Iran

.

Chanzo cha picha, Reuters

Katika muktadha wa mpango huo wa rais wa Marekani, gazeti la The Telegraph liliandika kichwa cha habari, “Hata kama Trump hawezi kupata amani, kuachiliwa kwa mateka ni ushindi.”

Gazeti hilo lilieleza siku ambayo mateka hao waliachiliwa huru kuwa “ya kipekee” kwa Trump na Israel.

Gazeti hilo lilibainisha kuwa ulikuwa ni “wakati mzuri” kwa Trump, ambaye jina lake “liliimbwa na umati wa watu huko Tel Aviv na Bunge la Israel lilikuwa likijiandaa kumkaribisha kama shujaa asiye na kifani, lakini haswa kwa familia za mateka ambao walinusurika kwa siku 738 walizozuiliwa.”

Gazeti hilo liliongeza: “Yeyote aliyedhani Israel imetengwa na kutishwa na kushutumiwa kimataifa kwa vitendo vyake huko Gaza bila shaka alishangazwa na kujiamini na matumaini yaliyoonyeshwa katika bunge la Israel la Knesset.”

Lilibainisha kuwa Netanyahu “alipokea sifa, ingawa ushughulikiaji wake wa mgogoro huo haukupata kuungwa mkono kwa wingi” nchini Israel.

Katika muktadha huu, gazeti hilo lilisema kwamba “kiongozi wa upinzani wa Israel Yair Lapid aliwashambulia waandamanaji wa kila wiki dhidi ya Israel katika miji kama London, akisema walidanganywa kuamini kuwa kulikuwa na mauaji ya halaiki na njaa ya kimakusudi ya Wapalestina.”

Gazeti hilo lilinukuu kauli za Trump kuhusu Iran, mhusika mkuu pekee aliposema, “Nimezuiliwa kabisa kutengeneza silaha ya nyuklia.” Gazeti hilo lilibainisha kauli ya Trump kwamba kufikia makubaliano ya amani na Tehran itakuwa jambo la kipekee sana, na kudokeza kwamba angejaribu kufanya hivyo hivi karibuni.

Gazeti hilo lilizingatia kauli ya Trump kwamba hii ilikuwa ni mwanzo wa Mashariki ya Kati mpya “kabla ya wakati,” likitaja historia. Hata hivyo, lilisema kuwa Trump, baada ya juhudi alizofanya, ana kila sababu ya kutumaini hili.

Huko Sharm el-Sheikh, Misri, “Trump alitaka kufufua Mkataba wa Abraham, amani ya kudumu kati ya mataifa ya Kiarabu na Israeli, lakini maana ya yote haya kwa Wapalestina haijulikani,” gazeti hilo liliripoti.

Kuna uwezekano gani wa kufufua suluhisho la serikali mbili?

.

Chanzo cha picha, EPA

Katika gazeri la Washington Post, mwandishi Max Boot aliuliza, “Kwa nini usitishaji vita wa Gaza hautaleta amani ya kudumu?”

Mwanzoni mwa makala yake, mwandishi aliuliza, “Je, huu ni mwanzo wa Mashariki ya Kati mpya, au ni usitishaji mwingine wa mapigano katika mzozo wa Waarabu na Wayahudi ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka 100?”

Liliandikwa, “Dalili zote zinaonyesha kuwa hatujafikia mwisho wa suala la amani ya Gaza.”

Kubadilisha usitishaji mapigano kuwa amani ya kudumu kunahitaji “kujinyima” ambako sio Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu au kiongozi wa Hamas Khalil al-Hayya anayeonekana kuwa tayari kufanya hivyo, kulingana na mwandishi.

Alidokeza kuwa mwisho wa vita “unawakilisha fursa” ya kufufua suluhisho la serikali mbili.

Mpango wa amani wa Trump “umetoa mwanya kidogo wa kuanzishwa kwa taifa la Palestina-unazungumza juu ya kuunda mazingira ya njia ya kuaminika kuelekea kujitawala kwa Wapalestina na kuwa taifa,” mwandishi huyo alisema, lakini akaongeza, “Israel na Hamas zinaonekana kudhamiria kufunga mlango huo.”

Mwandishi aliamini kwamba sharti la kwanza la kuelekea amani ya kudumu ni kupokonywa silaha kwa Hamas. Hata hivyo, alisema kuwa Hamas, badala ya kuachana na silaha zake, kundi hulo limeibuka tena kuthibitisha udhibiti wake juu ya sehemu za Ukanda wa Gaza ambazo haziko tena chini ya utawala wa Israel, kwa mujibu wa mwandishi huyo.

Licha ya hasara kubwa ambayo Hamas iliipata wakati wa vita—ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa viongozi wake wengi na wapiganaji wakongwe—wanachama wake huko Gaza bado wanakadiriwa kuwa karibu 15,000, kulingana na mwandishi huyo.

Alilichukulia hili kama “tatizo kubwa la kutekeleza mpango uliosalia wa amani wa Trump,” na akasema kwamba nchi za Kiarabu “hazitatuma vikosi vya kulinda amani ikiwa italazimika kukabiliana na Hamas, na Israel na Marekani hazitaruhusu mtiririko wa fedha za ujenzi mpya ikiwa Hamas itazinyakua kama ilivyofanya huko nyuma.”

Baada ya Misri, Qatar na Uturuki kufanya kazi ya “kuvutia” kuishinikiza Hamas kukubali kusitishwa kwa mapigano na kuwaachilia mateka, mwandishi aliuliza, “Je, nchi hizi zitafanikiwa kushawishi Hamas kuachana na silaha zake?”

Mwandishi anaamini kwamba ikiwa nchi hizi zitashindwa kufanikiwa, “Gaza kuna uwezekano mkubwa wa kusalia kama Mogadishu kwenye Bahari ya Mediterania, na maono makuu ya Trump ya kuijenga upya hayatatimia.” Ameongeza kuwa “Wapalestina watakosa uwezekano wa kupata ustawi na hatimaye kupoteza uwezekano wa kupata mamlaka.”

Kinyume chake, “Netanyahu amedhamiria kuzuia suluhisho la serikali mbili,” kulingana na mwandishi.

“Wakati vita vikiendelea, serikali ya mrengo wa kulia ya Netanyahu ilifanya kila inachoweza isipokuwa kunyakua rasmi Ukingo wa Magharibi… Ingetwaa Ukingo wa Magharibi rasmi kama Trump hangeizuia,” mwandishi huyo alisema.

Mwandishi huyo alionya kuhusu hatua za Israel zinazoweza kuzuia kuanzishwa kwa taifa la Palestina, ikiwa ni pamoja na “ujenzi wa makazi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, uhamisho wa vikosi vya Israel kwenye kambi tatu kuu za wakimbizi wa Palestina, na jitihada ndogo za kukomesha vurugu za walowezi kuwafukuza Wapalestina 3,000 kutoka kwa ardhi zao.”

Alidokeza kuwa “serikali ya Netanyahu inafanya kila inaloweza kuinyima Mamlaka ya Palestina mapato ya kodi na kuidhoofisha kwa kila njia,” ingawa mpango wa Trump unajumuisha maono ambayo Mamlaka hiyo itaidhibiti Gaza baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *