Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, amewataka watumishi wa umma na Watanzania kwa ujumla kufanya mazoezi, kula mlo sahihi na kupumzika vya kutosha ili kulinda afya za miili na akili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu “From Muscle to Brain” kilichoandikwa na Dkt. Catherine Kahabuka, Dkt. Shekalaghe amesema afya bora ni msingi wa utendaji kazi mzuri na ustawi wa jamii.
Kwa upande wake mtunzi wa kitabu hicho, Dkt. Catherine Kahabuka, amesema lengo la kitabu cha From Muscle to Brain ni kuwahamasisha watumishi wa umma na sekta binafsi kutumia taaluma na ubunifu wao kuunda fursa nje ya ajira rasmi, badala ya kutegemea ajira pekee.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates