KUTOKA DUBAI: Tazama namna Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Luten Jenerali Mstaafu Yacoub Mohammed aliv...

KUTOKA DUBAI: Tazama namna Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Luten Jenerali Mstaafu Yacoub Mohammed alivyoagana na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, viongozi pamoja na Watanzania wengine wakati msafara mzima wa kikosi hicho ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai kabla ya kuianza safari ya kurejea Tanzania.

Msafara huo unarejea nyumbani ukipitia Zanzibar na baadae kumalizia safari mwisho Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam leo.

Jana Oktoba 14, Stars ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Iran na kupoteza kwa jumla ya magoli 2-0.

#MechiYaKirafiki #IranVsTanzania #Iran #Tanzania #IRNTAN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *