Nyota wa Napoli, Romelu Lukaku amesema kuwa yeye na mdogo wake Jordan Lukaku watashindwa kumzika baba yao Roger Lukaku kwa vile wamezuiwa kuupeleka mwili wake Ubelgiji.

Rodger Lukaku (58), alifariki dunia mwezi uliopita jijini Kinshasa, DR Congo ambako pia mazishi yake yamepangwa kufanyika.

Tangu alipofariki, Watoto wake, Jordan na Romelu wamekuwa wakipambana kupata idhini ya kuuzika mwili wa baba yao huko Ubelgiji ambako aliishi kwa muda mrefu kabla ya kurudi DR Congo ambako mauti yamemfika.

Hata hivyo, hilo limeshindikana baada ya baadhi ya ndugu zao waliopo DR Congo kugomea na kutaka mwili wa Roger Lukaku kuzikwa ndani ya ardhi alikozaliwa.

“Baba yetu amefariki Septemba 28 na sisi kama ndugu tumejaribu kila kitu kuuleta mwili wake Ulaya lakini tunahisi kwamba tumekwamishwa na baadhi ya watu.

“Kama baba yetu angekuwepo hapa leo, asingekubaliana na hili. Imevunja nyoyo zetu kwa kushindwa kumpumzisha baba yetu. Lakinj ku a hawakulitaka hilo.

“Tunafahamu sasa kwa nini baba yetu alituweka mbali na watu wengi,” amesema Lukaku.

Roger Lukaku ni miongoni mwa nyota walioitumikia vyema timu ya Taifa ya DR Congo na klabu mbalimbali hasa vya barani Ulaya.

Alianzia soka lake katika timu ya AS Vita kisha akajiunga na  Sports D’Abdijan ya Ivory Coast.

Mwaka 1990, Roger Lukaku alihamia Ubelgiji na akachezea Seraing, Germinal Ekeren, Mechelen na Oestende.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *