Thamani ya mauzo ya madini ya chuma ya Iran ilipanda hadi karibu dola bilioni 4 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2025, na kuashiria ongezeko la asilimia 26 ya mauzo hayo kwa mwaka.

Mafanikio hayo yanakuja licha ya miaka mingi ya vikwazo vya Magharibi vinavyolenga viwanda vya chuma vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa kutegemea wataalamu wa ndani, upanuzi wa minyororo ya uzalishaji wa ndani, na maendeleo ya teknolojia ya kiasili, Iran imeweza sio tu kuendeleza bali kupanua pato lake la chuma – ikiimarisha nafasi yake kama mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa chuma katika eneo hili.

Kiasi cha mauzo ya nje ya bidhaa za mnyororo wa chuma kiliongezeka kwa 34% katika kipindi hicho tajwa. Aidha jumla ya mauzo ya nje ya mnyororo wa madini hayo yaliongezeka kwa 45%.

Usafirishaji wa madini ya chuma nje ya nchi uliongezeka maradufu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Kiwanda cha chuma hapa Iran

Kwa mujibu wa takwimu za Jumuiya ya Madini Duniani, Iran imepanda ngazi hadi nafasi ya 8 katika uzalishaji wa chuma duniani.

Sekta ya chuma ya Iran ina jukumu muhimu katika mauzo ya bidhaa zisizo za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *