Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewasihi vijana na Watanzania kwa ujumla, kuepuka kushawishika na kuingia katika migogoro ya kisiasa ambayo inaweza kuhatarisha amani, mshikamano na mustakabali wa taifa.

Nape amesema hayo alipokutana na vijana wa vijiwe mbalimbali ndani ya Jimbo la Mtama na kuwasisitiza kutoingia katika ugomvi wa kisiasa kwani mara nyingi wanasiasa hao huja kupatana na kuwaacha wao wakiwa wameathirika bila msaada.

✍Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *