Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga uwanj…Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga uwanj…

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga uwanja wa ndege wa kisasa, miradi tisa ya maji na barabara za kiwango cha lami, wilayani Misenyi katika Mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, anafanya hivyo akilenga kuinua maisha ya Watanzania wanaoishi wilayani humo na kuujenga utu wa mtu kama ilivyo kaulimbiu ya chama hicho ya Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.

Rais Samia ametoa ahadi hizo leo, Jumatano Oktoba 15, 2025 alipozungumza na wananchi wa Misenyi mkoani Kagera, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Miradi tisa hiyo ya maji, amesema inatarajiwa kunufaisha maeneo ya Bugango, Buchurago, Bubale, Minziro, Bugorora, Ruzinga, Bugandika, Mushasha, Mwemage, Byeju, Kashyenye, Kanyingo na Mgana.

Mradi mwingine ni kuweka lami kilomita mbili katika Barabara ya Bulembo Kona hadi Hospitali ya Wilaya na kukamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Buyango ili vijana wapate ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa na kujiajiri.

Ujenzi wa soko la kisasa la Bunazi, mikopo kwa wananchi kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba katika Mwalo wa Kabindi na kupeleka miche milioni mbili ya kahawa na 500,000 ya parachichi ni ahadi nyingine alizozitoa kwa wananchi wa Misenyi.

“Ukifika Zanzibar has akule Pemba, harufu inayokukaribisha ni ya karafuu. Nilipoingia hapa Misenyi nilikaribishwa na harufu ya Kahawa, nikasema eeh nimeingia kwenye eneo la kahawa,” amesema.

Dkt Samia amesema atakamilisha ujenzi wa Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 18, limegharibu Sh31.5 bilioni.

Ameeleza ujenzi huo utawarahisishia wakulima wa miwa kusafirisha miwa kutoka mashambani hadi kiwandani, kutoka zaidi ya kilomita 100 hadi kilomita 14 pekee.

Ameahidi pia kutekeleza ujenzi wa Barabara kutoka Kibaoni Bunazi na Kagera Sugar Junction kwa Sh54.7 bilioni na barabara ya Ketema-Katoro-Kyaka ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *