Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ametaka maandalizi ya kila mwananchi kujua kituo chak…Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ametaka maandalizi ya kila mwananchi kujua kituo chak…

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ametaka maandalizi ya kila mwananchi kujua kituo chake cha kupigia kura yaanze sasa, ili kuepusha usumbufu siku ya uchaguzi.

Katika msisitizo wake kuhusu hilo, Samia amesema wananchi wamerahisishiwa mazingira ya kupiga kura, hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Oktoba 15, 2025 alipozungumza na wananchi wa Kayanga mkoani Kagera, katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Amesema itakapofika siku ya uchaguzi, kila mwananchi amhamasishe ndugu na jamaa yake aliyejiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, kwenda kupiga kura.

“Matayarisho ya kutoka kwenda kupiga kura yaanze sasa, kila mtu ajue kituo chake, kila mtu ajue kapangwa wapi kwenda kupiga kura ili siku ile unajua natoka nyumbani nakwenda mahali fulani kupiga kura,” amesema Dkt Samia.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *