Mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuongeza uzalishaji wa miche ya kahawa na kutoa matrekta kwa wakulima wa Kagera kwa gharama nafuu, ili kuongeza tija kwenye kilimo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni Muleba, Dkt. Samia amesema serikali itaendeleza ruzuku za mbolea na pembejeo, pamoja na programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) inayowawezesha vijana kushiriki katika kilimo, ufugaji na madini.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *