Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amewahakikishia wazee na wananchi wa mkoa huo usalama na amani wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.

Akizungumza katika matembezi ya amani ya wazee wa Arusha, yaliyofanyika kwa ajili ya kuliombea Taifa amani na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Makalla ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kupiga kura kwa wingi na kudumisha utulivu kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Amesema amani ni nguzo ya maendeleo na sekta ya utalii katika mkoa huo.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *